Bosi na Kocha wa Timu ya
Arsenal Arsene Wenger amesema Tottenham
ilistahili ushindi katika mechi iliyochezwa leo April 30 kati ya Arsenal na
Tottenham ambapo Tottenham imeigaraza timu ya Arsenal kwa Magoli mawili kwa
bila
Arsene Wenger aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na BBC
mara baada ya mchezo huo kuisha “tumepoteza mchezo huu, na itatuchukua muda
kujiweka sawa, lakini kiujumla Tottenham walistahili ushindi, inatubidi
tukubali na tulitafakari zaidi, japo inakatisha tamaa lakini lengo letu la
mwanzo katika msimu huu ni kushinda katika ligi” Alisema Wenger
Timu ya Tottenham ilijipatia
ushindi wake kupitia wachezaji wake machachari kabisa Harry Kane na Dele Alli na
kuweka historia ya kuwa juu nafasi nne zaidi ya timu ya Arsenal katika msimamo
wa ligi kuu Uingereza, ambapo hivi sasa Spurs ikishika nafasi ya pili kwa jumla
ya Pointi 77 huku Arsenal ikiwa na pointi 60.
Naye meneja wa timu ya
Tottenham Spurs Mauricio Pochettino alizungumza haya, “huu ulikuwa mchezo muhimu sana na wachezaji
wameonesha mchezo mzuri, nimefurahishwa”, “tulikuwa vizuri katika kipindi cha
pili, tuliweka nguvu kubwa na kutengeneza nafasi zaidi”
0 comments:
Post a Comment