ALBERT MSANDO AMEOMBA RADHI KUFUATIA VIDEO YAKE NA GIGY MONEY INAYOSAMBAA MITANDAONI

Mwanasheria maarufu nchini Tanzania Albert Msando ameomba radhi kufuatia video inayosambaa mitandaoni ikionesha Mwanasheria huyo akiwa na Gigy Money ndani ya gari, ambapo Albert ameonekana akimpapasa mwanadad huyo Gigy alipokuwa akicheza muziki kwa madoido.

Msando ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema kwamba akikaa kimya atakuwa manafiki kwa kuwa kitendo alichokifanya hakiwapendezi wengi kwani kimewakwaza na kuwaangusha watu wengi japo alisema yeye ni binadamau ingawa wapo watu ambao wanaweza kuhukumu kwa haraka zaidi.
“Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship” ameandika Albert.  
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment