RAIS MAGUFULI AMTEUA ADOLF NDUNGURU KUWA NAIBU KAMISHNA WA TRA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa naibu kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), ambapo uteuzi huo umeanza leo Mei 22 2017.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Adolf Ndunguru alikuwa kamishna wa sera katika wizara ya fedha na mipango.
Bw. Adolf anachukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Bw. Charles Kichere ambaye naye aliteuliwa kuwa kamishna mkuu katika mamlaka hiyo. 

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment