Huko nchini Kenya Rais wa
nchi hiyo Uhuru Kenyatta amesaidini muswada utakaowawezesha wananchi wake
kukopa kwa kutumia mifugo, mimea na vitu vya nyumbani kama dhamana ya kupata
mikopo. Muswada huo umewalenga wale ambao hawana umiliki wa gari, ardhi ama
nyumba kama dhamana ya kupata mkopo.
Sheria hiyo itakayojulikana
kama “Movable Property Security Act 2017” itatoa fursa ya usajili wa mali
ambazo zitatumika kama dhamana ya kupatia mkopo benki, kutokana na kwamba benki
zimekuwa zikikataa kutumia mali zinazohamishika kama dhamana ya kupatia mikopo
kutokana na kutokuwepo kwa taarifa sahihi za mali hizo zitakazwawezesha kudai
mali hizo pindi mdaiwa atakaposhindwa kulipa mkopo.
Rais Kenyata amesema sharia hiyo
italeta udhibiti wa uhakika kwa kutoa dhamana ya mali lakini pia itabainisha ni
mali gani itafaa kutumika kama dhamana.
0 comments:
Post a Comment