Maelfu ya wakazi wa jiji la
Arusha wamehudhuria shughuli ya uagaji miili ya wanafunzi 32 wa darasa la saba,
walimu wawili na dereva wa shule ya Lucky Vicen katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid mkoani Arusha waliopata ajali ya gari katika eneo la Rhotia Marera
wilyana aratu walipokuwa wakisafiria kwenda shule ya jirani iitwayo Tumaini kwa
ajili ya kufanya mitihani ya ujirani mwema.
Shughuli hiyo iliyoongozwa
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa
niaba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli.
Mkamu wa Rais amewaomba
wananchi katika kuwaombea marehemu Mung4u awaaze mahala pema peponi a kuwafariji
wafiwa katika wakati huo mgumu. Lakini Pia Makamu wa Rais amewahakikishia ndugu
na wanafamilia wa marehemu kuwa serikali iko pamoja nao.
Makamu wa Rais katika hotuba
yake amaeitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Polisi, walimu wazazi na
walezi kuhakikisha sharia za usalama barabarani zinafuatwa na kuzingatiwa ili
kulinda watoto pale wanapokuwa katika vyombo vya usafiri. Piaa amewataka
madereva nchini kuzingatia sharia za usalama barbarani na kuacha tabia za
ulevi wa kutumia pombe na dawa za
kulevya ili kuepusha kutokea kwa ajali za mara kwa mara.
Shughuli hiyo imehudhuriwa
na viongozi mbali mbali wakiwemo viongozi wa kidini na kiserikali, akiwemo
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Pili wa Serikali ya
Zanzibar Mohamed Aboud na viongozi wengine wa vyama vya siasa na dini
mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment