Kiungo wa timu ya mpira wa
miguu Simba Sposts Club Jonas Mkude amenusurika kifo kufuatia ajali ya gari
iliyotokea leo katika eneo la Dumila Mkoani Morogoro akitokea Dodoma kwenda
Dar. Nahodha huyo wa timu ya Simba SC amepatiwa huduma ya kwanza na kuwahishwa
hospitalini jijini Dar kwa matibabu zaidi.
Ajali hiyo imetokea baada ya
tairi la nyuma la gari aina ya Toyota VX yenye namba za usajili T 834 BLZ waliyokuwa
wakisafiri, kupasuka na kuacha
njia, majeruhi wengine wawili wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro
kwa matibabu
0 comments:
Post a Comment