RAIA WA KOREA KUSINI KUMCHAGUA RAIS MPYA LEO

Raia wa Korea Kusini leo Mei 9 2017 wanamchg4ua Rais mpya atakayeiongoa nchi hiyo kwa awamu inayofuata, ambapo uchaguzi huo unafanyika baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya ulaghai kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Park Geun Hyu.

Uchaguzi wa awamu hii huko Korea Kusini wenye wagombea kumi na watatu unatarajiwa kuwa na ushiriki wa watu wengi kwenye kupiga kura huku wengi wao wakiwa ni vijana
Mmoja wa wagombea wa kiti hiko kutoka chama cha Liberal, Moon Jae-In alisema anataka kuimarisha mahusiano ya nchi hiyo na Korea Kaskazini baada ya mahusiano ya nchi hizo mbili kuzorota huu Ahn Cheol-soo ambaye ni mpinzani mkuwa wa Moon amepingana na mawazo hayo.

Korea Kusini na Korea Kaskazini zimekuwa katika hali ya mahusiano ya kutoridhisha kwa muda kufuatia vitendo vya Korea Kaskazini ya kufanya uzalishaji na majaribio ya mara kwa mara ya silaha za nyukli.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment