CHELSEA YAIBAMIZA MIDDLESBROUGH 3 BILA

Timu ya Chelsea ya mjini Uingereza imeichapa bao tatu kwa bila timu ya Middlesbrough katika mchezo uliochezwa jana Mei 8 katika Uwanja wa Stamford Bridge.

Bao la kwanza la Chelsea lilitiwa wavuni na Mchezaji machachari kabisa Diego Costa baada ya kuiotea pasi nzuri kabisa kutoka kwa mgonga pasi Cesc Fabregas mnamo dakika ya ishirini na tatu ya mchezo huo. Marcus Alonso alinogesha mchezo huo na kuwafurahisha mashabki wa timu hiyo ya The Blues baada ya kuunyaka mkwaju murua na kuiwezesha Chelsea kujipatia bao lake la pili mnamo dakika ya 34 huku mchezaji Matic akiipatia Chelsea bao lake la tatu katika dakika ya 20 ya kipindi cha pili.

Kufuatia mchezo wa jana Chelsea inaendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza kwa kuwa na jumla ya pointi 84.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment