ANTONIO KONTE; TUNASTAHILI KUSHINDA LIGI KUU YA UINGEREZA

Meneja wa timu wa timu ya Chelsea Antonio Konte amesema wachezaji wake wa timu ya Chelsea wana nafasi nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza katika msimu huu.

Timu ya Chelsea imepata matumaini hayo baada ya mchezo uliochezwa jana kati yao na Middlesbrough na kushinda bao tatu kwa bila na kuiwezesha timu hiyo kupata jumla ya point 84 wakiwa wanaendelea kuongoza ligi hiyo ya Uingereza.
Konte aliiambia BBC katika mechi hiyo kuwa japo huu ni msimu wa kwanza kwake na umekuwa na ushindani mkali katika ligi hiyo lakini wchezaji wake wameonesha kwamba wanastahili kushinda ligi msimu huu

“huu ni msimu wangu wa kwanza, na umekuwa na ushindani mkali,nimefurahishwa na wachezaji wanastahili, tumeonesha kwamba tunastahili kushinda ligi” alisema Konte 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment