Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe
Magufuli ametoa msaada wa magari mapya aina ya Land Cruiser kwa ajili ya
kubebea wagonjwa kwa wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa maeneo wanayoyaongoza.
Katibu kiongozi mkuu Mhe. Balozi John Kijazi akimkabidhi Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Keissy fungu ya gari kwa ajili ya kubebea wagonjwa jimboni kwake
|
Katibu mkuu kiongozi Balozi JoHn Kijazi amekabidhi magari
hayo kwa niaba ya Rais Magufuli Ikulu
jijini Dar es salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini mkoa wa Katavi Mhe. Ally
Keissy, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa
viti maalum mkoa a Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga.
Akizungumza baada ya kukabidhi magari hayo Balozi Kijazi
amesema Mhe. Rais Magufuli ametoa magari hayo baada ya kuguswa na kilio cha
muda mrefu cha wabunge hao waliokuwa wakiomba wananchi wao wapatiwe magari ya wagonjwa.
“Mhe. Rais ameamua kuwakabidhi nyinyi haya magari kutokana na vilio vyenu ambavyo amekuwa
akivisikia mara kwa mara, Mhe Keissy amekuwa hata akitafuta miadi ya kuja
kumuona Mhe. Rais kwa suala hili, Waheshimiwa wabunge wamekuwa wakiyazungumza
haya kwa muda mrefu”
Wabunge hao walimshuru Rai wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo wa magari kwa ajili ya kubebea
wagonjwa na kusema kuwa Rais ameonesha upendo na kuwajali wananchi wake kwa
kutekeleza yale aliyoahidi
“Kwa wananchi na wanamkoa wa Shinyanga hususani akinamama
wa mkoa wa Shinyanga mimi kama mwakilishi wao mbunge wa viti maalum mkoa wa
Shinyanga nasema namshukuru sana Mhe Rais anaendelea kutekeleza yale ambayo
anayoyaamini na anaendelea kuonesha upendo wake mkubwa sana kwa wananchi kwa
vitendo” alisema Lucy Mayenga
0 comments:
Post a Comment