Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa mkuu wa
mkoa wa Arusha Ndg. Mrisho Gambo kufuatia ajali ya basi iliyotokea leo saa tatu
asubuhi katika eneo la Rhotia Marera wilayani Karatu na kusababisha vifo vya
wanafunzi wa darasa la saba 32, dereva na walimu wawili wa Shule ya Lucky
Vicent iliyoko mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao
walikuwa wanatoka shuleni kwao na kwenda shule ya msingi Tumaini kwa ajili ya
kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofikka eneo la Rhotia Marera basi
walilopanda liliacha njia na kasha kutumbukia kwenye Korongo na kusababisha
vifo hivyo.
0 comments:
Post a Comment