Chama cha Mapinduzi kimesema
kuwa zoezi la kuwafukuza wasaliti kwenye chama hiko kwa sasa linakwenda kwenye
ngazi ya mashina na tawi ili kuhakikisha chama kinabaki na watu waaminifu na
wema.
Maneno hayo ameyazungumza
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Alhaji Abdallah Bulembo alipokuwa
akizungumza na wanachama wa CCM wilaya ya Ilala katika ziara yake mkoni Dar es
salaam.
“Kwanini tumepoteza madiwani
ni usaliti tulioutengeneza ndani ya Chama chetu, kuwa CCM ni imani, kuwa
muislam ni imani, na kuwa mkristo ni imani, sasa unapoona imani yako wewe ina
utata kama unataka kwenda wewe nenda si ndio jamani, watakao kuwa na imani watazidi
kubaki na imani yao,” alisema Bulembo.
Bulembo ameongeza kwa kusema
anatambua kuwa Dar es salaam kuna shida na kuahidi kwamba kabla uchaguzi
kumalizika uhakiki wa wasaliti wa chama utakuwa umekwishafanyika
“Kwahiyo kwa Dar es salaam
tunayoshida na niliseme moja kwa moja hapa na popote ntakapo kwenda ntasema
kabla ya agenda yangu kubwa ya uchaguzi Dar es salaam hatujamaliza na naomba
nieleweke vizuri Dar es salaam hatujamaliza kuwahakiki waliokuwa wasaliti, tutakuja
hadi kwenye matawi.” alisema Bulembo
0 comments:
Post a Comment