IDADI YA WALIOFARIKI KWENYE AJALI ARUSHA YAFIKIA 33

Idadi ya wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent waliofariki katika ajali huko Karatu mpaka sasa ni 33, ambapo wasichana ni16, na wavulana 17. Waliofariki wengine ni watu wazima wane. Ajali hiyo I imetokea leo asubuhi katika eneo la Marera , Karatu mkoani Arusha.

Wazazi wa wanafunzi tayari wameanza kufika katika shuleni Lucky Vicent Nursery and Primary School ili kupata taarifa zaidi.

Baadhi ya wa wanafunzi wakiwa wamewasili Shuleni Lucky Vecent kwa taarifa zaidi kufuatia ajali iliyotokea na kuua wanafunzi wa shule hiyo


Basi lililokuwa limepakia wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent likiwa limeharibiwa vibaya kna ajali iliyotokea
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment