Mbunge wa
jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema kuwa amefurahishwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa ni mwenye kusikia vilio vya watanzania
wanyonge. Hayo ameyasema jana katika ukurasa wake wa Instagram kufuatia suali
alilouliza Bungeni kwa wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango juu ya hali ya uchumi
ambayo inawabana watu wa chini.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete |
Mbunge huyo
amejaribu kueleza namna mbali mbali ambazo zinaweza kuiezea mapato serikali
bila ya kuwabana watu wa kipato cha chini, ikiwemo kupitia benki ya Uwekezaji
TIB(Tanzania Investment Bank), TIBD (Tanzania Investment Development Bank) na
miradi mbalimbali ukiwemo ule wa umeme wa bwawa la Kidunda,
Kufuatia hoja
hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
ghafla ya ufunguzi wa mfumo mpya wa ukusanyaji kodi alisema kwamba anashangazwa
kuona kuna wataalamu wengi wa uchumi lakini wanafikiria kuongeza kodi badala
ya kufikiria namna nyingine ya kuongeza mapato ya nchi.
"Tuna
wachumi wengi wamekaa tu. Wao wanawaza kupandisha kodi ya bia. Hawawazi nje ya
mipaka namna mpya ya kuongeza mapato" amesema Rais Magufuli
Hoja hiyo ya
Mbunge Ridhiwani imeonesha kuleta matumaini kwa kuwa ni miongoni mwa hoja
ambazo Rais Magufuli amezisemea mapema zaidi mara baada ya kusikika bungeni.
0 comments:
Post a Comment