Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki |
Serikali kupitia Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza ajira 10,184
ikiwa ni vibali vya ajira kwa taasisi za umma, mashirika ya umma, serikali za
mitaa, sekretarieti za mikoa, na wakala wa serikali ili kujaza nafasi
zilizoachwa wazi kufuatia zoezi la uhakiki wav yeti feki ambalo liliwatoa
watumishi takribani 15,000 kazini na kuacha nafasi hizo wazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki
ametangaza ajira hizo jana alipokuwa katika kikao na watumishi wa Umma wa
Wilaya ya Kigamboni, amesisitiza pia kwa kusema kuwa utoaji wa vibali hivyo vya
ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la vyeti
feki kwa watumishi wa umma kote nchini.
Waziri Kairuki ameongeza
kuwa mpango wa Serikali wa kutoa ajira mpya bado upo pale pale na kuwa hawa
watakaoajiriwa kujaza nafasi hizo watatakiwa kuripoti vituo vyao vya kazi mwezi
Agosti mwaka huu. Utaratibu wa
kukamilisha idadi ya waajiriwa 15,000 wa nafasi zilizoachwa kutokana na zoezi
la vyeti feki unaendelea ambapo mgao wa vibali vya ajira 4,816 ili kukamilisha
nafasi 15,000.
0 comments:
Post a Comment