Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Sion Sirro amefanya mabadiliko ya baadhi ya maofisa wa jeshi la
polisi kwa kuwabadilishia sehemu za kazi maofisa hao. Maabadiliko hayo
yamewahusisha kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Kamanda wa
polisi Mkoa wa Mbeya.
Ambapo aliyekuwa Kamanda wa
Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu kamishna wa Polisi Mohammed Mpinga
amebadilishwa nafasi yake na kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya huku nafasi
yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu.
Pia mabadiliko hayo
yamemhusisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri
Kidavashari ambaye amehamishiwa makao makuu ya Jeshi la Polisi.
0 comments:
Post a Comment