Kilabu ya Soka ya nchini
Uingereza Everton imetua jijini Dar es salaam leo asubuhi kuikabili timu ya Gor
Mahia kutoka nchini Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa
siku ya Alhamis Julai 13 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Jopo la timu hiyo wakiwemo wachezaji
hao na wakufunzi pamoja na maafisa wengine wa timu walifika uwanja wa ndege saa
mbili asubuhi kutoka Liverpool. Mashabiki wengi wa soka ya England wamesafiri
Tanzania kushuhudia Everton wakichuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika
uwanja wa taifa wa michezo jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Timu ya Everton wakielekea kwenye basi mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere
|
Timu hiyo inaingia dimbani
katika uwanja wa taifa ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kumchezesha
mchezaji wake mpya straika Wyne Rooney ambaye amajiunga na timu yake hiyo ya
zamani siku chache tu zilizopita akitokea Manhcester United ambako alikuwa
akichezeka kwa kipindi cha miaka mitatu.
Timu hizo zote mbili, Gor
Mahia ya Kenya na kilabu ya Everton zimewasili jijini Dar es salaam, huku timu
ya Eeverton ikikaribishwa leo hii asubuhi na Waqziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe mara baada ya kutua katika uwanja wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere International Airport.
Naye aliyekuwa nahodha wa Manchester United Wyne Rooney ameeleza kuwa amaefurahishwa na ujio wake nchini Tanzania kwa kuwa atapata fursa nzuri ya kuwatambua wachezaji wenzake wa timu hiyo ya Everton ambako maliko kwa sasa.
Mashabiki wa timu ya Everton
wakipiga piacha na wachezaji wa timu hiyo akiwemo Rooney
|
Wachezaji wa timu
ya Everton wakiwa katika hoteli waliyofikia jijini Dar es salaam
|
Wachezaji wa timu ya Everton wakiwa katika shule ya
Msingi Uhuru Jijini Dar es salaam
|
Wachezaji wa timu ya Everton wakisalimiana na wanafunzi wa shule ya
Msingi Uhuru Jijini Dar es salaam
|
0 comments:
Post a Comment