Wabunge kumi na madiwani wawili wa Chama cha wananchi CUF wasusia
Kikao, viongozi hao wa Chama cha Wananchi (CUF) waliitwa leo kwa ajili ya
mahojiano katika Ofisi za Chama hiko bila kutokea.
Wabunge
hao wanaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad waliitwa ili
kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuhusu mgogoro
unaoendelea.
Katika
taarifa iliyotolewa jana na chama hicho upande unaomuunga mkono, Mwenyekiti
Profesa Ibrahim Lipumba uliwataka viongozi hao kufika katika ofisi hizo saa
3.00 asubuhi leo lakini mpaka kufikia saa 6:00 mchana walikuwa bado hawajafika.
Mbunge
wa viti maalum wa chama hicho aliyeitwa kwenye mahojiano hayo, Severina Mwijage
amesema hana taarifa za kuitwa kwenye kikao hicho.
“Niko safarini Bukoba sifahamu kuhusu kuwepo kwa kikao hicho,” amesema Mhe Mwijage kwenye mahojiano
yake na Gazeti la Mwananchi.
Mbunge
mwingine wa viti maalum wa chama hicho, Mgeni Kadika amesema alipata taarifa za
kuwepo kwa kikao hicho lakini hatahudhuria.
“Nilipata taarifa kupitia ujumbe mfupi (SMS) lakini sitafika kwenye kikao
hicho kwa kuwa nauguliwa na watoto huku Pemba,” amesema Kadika.
0 comments:
Post a Comment