LIVERPOOL YAIBUKA BINGWA BAADA YA KUIBAMIZA LEICESTER

Timu ya Liverpool nchini Uingereza imeibuka mshindi wa kombe la Asia awamu ya 2017 bada ya kuifunga Leicester goli 2-1 mjini Hong Kong.
Mohamed Salah na Phil Coutinho walifunga mabao mawili na kuishinda Leicester waliokuwa wamefunga bao la mapema.
Huku kukiwa na uvumi kwamba Coutinho huenda akajiunga na Barcelona haikutarajiwa kwamba nyota huyo wa Liverpool angefunga bao la ushindi.
Mechi ilikuwa na kipindi cha kwanza cha kutumbuiza huku washambuliaji wote wa timu hizo wakishiriki.
Coutinho na Salah walikuwa wakionana kwa kipindi kirefu cha mechi.
Leicester ndio ilioanza kufunga baada mchezaji Fuchs kutumia wingi ya kulia kabla ya kupiga krosi nzuri kwa Isaac Slimani ambaye alifunga kwa kichwa katika dakika ya 12 kipindi cha kwanza


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment