Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa ametoa miezi mitatu kwa wananchi wote waliojenga ndani ya eneo
la mpaka wa Tanzania na Zambia kubomoa nyumba zao na kuiagiza Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kuanza kuweka alama za kubomoa (alama za X) katika nyumba 252
zilizojengwa ndani ya mpaka huo ili wahusika wazibomoe.
Agizo hilo
amelitoa alipotembelea eneo la ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha (OSBP)
katika mpaka wa Tanzania na Zambia, ambacho kinajengwa na Serikali ya Tanzania
na kitagharimu sh. bilioni 12.
“Kuna watu
wamejenga ndani ya mpaka wa Tanzania na Zambia na kuendesha biashara zao jambo
ambalo ni kinyume cha sheria na linazikosesha Serikali mapato.”Kufuatia hatua
hiyo Waziri Mkuu ametoa muda wa miezi mitatu kwa watu wote waliojenga kuanzia
umbali wa mita 50 kutoka Tanzania na mita 50 kutoka Zambia kuzibomoa nyumba
hizo kwa hiari.
“Hatuna
msamaha kwa watu waliojenga katika eneo hili kwa sababu wamesababisha tupoteze
kodi nyingi, hivyo baada ya kumalizika muda huo mamlaka husika zibomoe nyumba
zote zitakazosalia.”
Awali Waziri
Mkuu alikutana na Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchini Zambia, Bw. Field Simwinga
ambaye alisema wamekubaliana na utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa jambo hilo
linaathiri shughuli za mipakani kwa pande zote mbili.
Bw. Simwinga
alisema tayari wameshaanza kuwaeleza wananchi wao waliojenga ndani ya mpaka huo
kuanza kuondoka, ambapo Waziri Mkuu amesema wanataka eneo hilo liwe wazi ili
iwe rahisi kuutazama mpaka huo kwa umakini.
Mkuu huyo wa
wilaya ya Nakonde alisema utekelezaji wa jambo utafanikiwa kwa urahisi kutokana
na ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Zambia
0 comments:
Post a Comment