Chama cha Mapinduzi
(CCM) kimewaita wanafunzi wote wa elimu ya juu nchini ambao wamekosa
mikopo ya elimu yajuu kutokana na sababu mbalimbali, chama hiko kimewataka
wanafunzi hao kufika katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba
jijini Dar es Salaam. Katika taarifa
iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey
Polepole iliwataka wanafunzi wote ambao ni yatima, wenye ulemavu na ambao
wazazi wao ni walemavu lakini wamekosa mkopo wamefika katika ofisi za CCM.
Taarifa hiyo
iliyotolewa Julai 20 mwaka huu haikufafanua zaidi ni hatua gani
zitakazochukuliwa ili kuweza kuwasaidia wanafunzi hao walioitwa.
Akizungumzia hatua
hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO),
Stanslaus Kadugazile alisema hilo ni jambo jema na kwamba ni la kupongezwa zaidi
kwa kuwa wamewaita wote bila kuwabagua kivyama.
0 comments:
Post a Comment