Nchi ya Marekani kupiga marufuku raia
wake kusafiri kwenda nchini Korea Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na mashirika mawili yanayofanya kazi ya kupanga safari za kwenda nchini Korea
Kaskazini japo Seriakli ya Marekani bado haijathibitisha taarifa hizo.
Mashirika hayo ya Koryo Tours na Young Pioneer Tours yamesema
marufuku hiyo itatangazwa tarehe 27 Julai na itaanza kutekelezwa siku 30
baadaye. Shirika la Young Pioneer Tours ndilo lililofanikisha mwanafunzi Mmarekani
Otto Warmbier kuzuru Korea Kaskazini ambaye likamatwa baadaye muda mfupi kabla
yake kuondoka nchini humo na kuhukumiwa kufungwa jela miaka 15.
Hata hivyo, alirejeshwa Marekani mwezi Juni akiwa amepoteza
fahamu na akafariki dunia wiki moja baadaye.
Shirika hilo, lenye makao yake China, imesema haitasaidia
Wamarekani wengine kuingia Korea Kaskazini. Shirika hilo lilitoa taarifa Ijumaa
na kusema: "Tumefahamishwa sasa hivi kwamba serikali ya Marekani
haitawaruhusu tena raia wa Marekani kusafiri DPRK (Korea Kaskazini).
"Inatarajiwa kwamba marufuku hiyo itaanza kutekelezwa
katika kipindi cha siku 30 kuanzia Julai 27. Baada ya kipindi hicho cha siku 30
raia yeyote wa Marekani ambaye atasafiri Korea Kaskazini atafutiwa pasipoti
yake na serikali ya taifa lake."
Rowan Beard, wa Young Pioneer Tours, wameliambia shirika la
utangazaji la Uingereza BBC kuwa shirika hilo limefahamishwa hayo na ubalozi wa
Sweden, ambao hushughulikia masuala ya Marekani nchini Korea Kaskazini, pia
ubalozi huo unajaribu kujua idadi ya watalii kutoka Marekani ambao bado
hawajaondoka Korea Kaskazini.
Bw Beard amesema ubalozi huo unawahimiza raia wa Marekani
kuondoka nchini humo mara moja, amesema nafuu hiyo ya siku 30 "itawapa
fursa (Wamarekani) wowote ambao kwa sasa wamo nchini humo kama watalii ama
wakifanya kazi za kibinadamu."
Naye Simon Cockerill, wa Koryo Tours, ameliambia Shirika la
Utangazaji la Uingereza BBC kuwa amepashwa habari na ubalozi wa Sweden, amesema
shirika hilo bado litaendelea kupanga safari na kupeleka Wamarekani Korea
Kaskazini hadi marufuku hiyo ianze kutekelezwa.
"Ni habari za kusikitisha sana kwa sekta hii na pia kwa
raia wa Korea Kaskazini ambao wanataka kuwafahamu zaidi Wamarekani|” amesema Bw
Cockerill
0 comments:
Post a Comment