WAWILI WAFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA DALADALA

Watu wawili wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha daladala yenye namba za usajili T427 BQZ inayofanya safari zake kati ya Buza na Gerezani Kariakoo na treni ya TAZARA, ambapo Daladala hiyo iliigonga treni eneo la Devis Kona jijini Dar es salaam

Mkuu wa kituo cha polisi Ilala amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mpaka sasa watu wawili wamepoteza maisha huku wengine 30 wakiwa wamejeruhiwa na kupelekwa kupatiwa matibabu. Inadaiwa watu wanne wapo katika hali mbaya zaidi
“Majeruhi wite wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na miongoni mwa majeruhi hao wanne wapo katika hali mbaya”amesema Kamanda Muroto.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment