Baraza la Uongozi la Chama
Cha Mawakili wa Tanganyika (Tanganyika Law Society TLS) kimesema kuwa kimelaani
kitendo cha jeshi la polisi kumkamata na kuendelea kumshikilia Rais wa Chama
hiko cha Mawakili Mhe. Tundu Antipus Lissu jana jioni akiwa uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere alipokuwa akijiandaa kuelekea nchini Rwanda
kuiwakiloisha TLS kwenye kikao cha Braza la Chama cha Mawakiliwa Africa
Mashariki ambacho kinafanyika leo.
Mhe. Tundu Lissu
anashikiliwa na Polisi kwa makosa ya uchochezi ambayo tayari alionywa na
serikali kuacha kuendelea kutoa kauli za uchochezi na kupotosha umma.
Chama hiko Cha Wanasheria
kimetoa wito kwa Jeshi la Polisi kumpatia Dhamana Mhe. Tundu Lissu pamoja na
kumfikisha mahakamani ndani ya muwa wa kisheria kama ambavyo sharia za nchi
zinavyoelekeza.
0 comments:
Post a Comment