Zanzibar imefutiwa uanachama
wake katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ikiwa ni miezi minne tu imepita
tangu walipokubaliwa na kuwa mjumbe wa shirikisho hilo.
Rais wa CAF, Ahmad Ahmad
amesema kwa, Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania haikupaswa kabisa kukubaliwa
kuwa mjumbe wa 55, uamuzi uliofanywa Machi 2017.
Rais huyo amesema kuwa, Zanzibar
ilikubalia kuwa mwanachama wa CAF bila kuzingatiwa kwa vigezo vya msingi
ambavyo ni muhimu, huku akifafanua zaidi kuwa, CAF haiwezi kuvikubalia vyama viwili
vya soka kutoka nchi moja.
Rais wa CAF ameongeza kuwa
wamechukua uamuzi huo kwakuwa hawawezi kuruhusu kuwa na vyama viwili kutoka
nchi moja (Yaani TFF na ZFA)
CAF imesema kuwa kigezo chao
cha kutambua nchi ni ile inayotambuliwa na Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Umoja
wa Mataifa (UN).
Licha ya kuwa Rais wa CAF
aliyepita, Issa Hayatou aliikubalia Zanzibar kuwa mwananchama, lakini
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilikataa kuifanya Zanzibar kuwa mwanachama.
Zanzibar ni sehemu ya
Tanzania lakini kwenye masuala ya mpira imekuwa ikijitegemea. Katika mashindano
ya kanda, imekuwa ikishiriki kama nchi.
0 comments:
Post a Comment