MAWAKILI WA LISSU WASOTA POLISI, WAZUILIWA KUMUONA MTEJA WAO.

Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema mpaka sasa hajaruhusiwa kumuona mteja wake licha ya kufika Polisi Makao Makuu tangu asubuhi.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Julai 21, Karume aliyekuwa na wakili mwingine wa Chadema, Peter Kibatala amesema wameambiwa Lissu hatapelekwa mahakamani kwa sasa kwa kuwa upelelezi haujakamilika.
“Tupo hapa tangu asubuhi, tunaambiwa hatuwezi kumuona kwa sasa, lakini jambo la kushangaza ni kuwa tunaambiwa hatapelekwa mahakamani kwa kuwa uchunguzi haujakamilika ingawa kosa bado halieleweki,” amesema.
Amesema polisi wamewaambia mawakili wa Lissu kuwa hata dhamana kwa leo haitawezekana kwa sababu upelelezi haujakamilika

Hata hivyo wakili Fatma Karume amesema wamepeleka maombi Mahakamani leo wakitaka Polisi wamfikishe Lissu kortini ili waache kumshikilia bila kumshtaki.
.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment