Rais wa Jamhuri ya Burundi
Mhe. Piere Nkurunzinza leo tarehe 20 Julai, 2017 amefanya ziara ya rasmi ya
kiserikali ya siku moja hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Johnh Pombe Magufuli.
Ziara hiyo imefanyika katika
wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambapo Mhe. Raios Nkurunzinza amepokelewa rasmi
kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa heshima yake katika eneo la Lemela na
baadaye mazungumzo rasmi na dhifa ya kitaifa iliyofanyika Ngara.
Akizungumza katika mkutano
huo Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amemshukuru Mhe. Rais
Nkurunzinza kwa kukubali mwaliko wake na amehakikisha kuwa serikali yake ya
awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria
na kindugu nan chi ya Burundi hususani katika kukuza Biashara na Uwekezaji.
“Tanzania ni ndugu zako na
watanzania ni ndugu wa watu wa Burundi, umekuja kwa mazungumzo ya kiuchumi,
tumezungumza mambo mengi ya kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Burundi,
katika takwimu za mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Burundi ilikuwa na
thamani ya Shilingi Milioni 116.5, kiwango hiki ni kidogo kwa nchi ya Burundi
ambayo ina watu Zaidi ya Milioni 10 na Tanzania ambayo ina watu Zaidi ya
Milioni 52” amesema Mhe. Rais Magufuli
Mbali na hayo Rais Magufuli
aliligusia suala la hali ya wakimbizi kutoka Burundi ambao walikimbilia nchini
Tanzania kipindi cha machafuko ya kisiasa. Rais Magufuli amesema kuwa
wakjimbizi waliokimbilia kutoka nchini Burundi ni wakati sasa kurudi nyumbani
kwani jitihada za Mhe. Rais Nkurunzinza za kulinda Amani zimeleta matunda.
Aidha Rais Magufuli
amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba kusitisha utoaji wa
uraia kwa wakimbizi hao ili utaratibu huo usitumike kama kigezo cha wao
kuzikimbia nchi zao.
Naye Mhe. Rais Nkurunzinza
amemshukuru Rais Magufuli kwa mwaliko na kutoa Wito kwa wafanyabiashara wa
Burundi na wafanyabiashara wa Tanzania kushirikiana katika biashara pia amesema
kuwa hali ya Burudni ni shwari kwani hata wakimbizi walioikimbia Burundi na
kukimbilia Tanzania miaka miwili iliyopita wanaendelea kurudi nchini Burundi na
kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo.
“Nataka kuwajulisha wenzetu
watanzania na waurndi wenzetu ambao walikimbilia Tanzania, Burundi la leo ni
nchi yenye Amani, tunawaalika Warundi wenzetu, kaka zetu, na dada zetu
waliokimbilia hapa Tanzania, warudi nchini kwao tujenge nchi yetu iwe na Amani ya
kudumu” amesema Rais. Nkurunzinza
0 comments:
Post a Comment