Spika WA Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ametangaza nafasi nane za ubunge ambazo
ziko wazi kuanzia sasa kufuatia kufutwa uanachama kwa wabunge hao na Mwenyekiti
wa Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba, Mhe Spika amemuandikia
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili aendelee na hatua zinazostahili
kujaza nafasi hizo kwa Mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo.
Wabunge hao wamefukuzwa
Uanachama kulingana na taratibu za Chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea
na Ubunge. Wabunge hao ni Mhe. Severina Silvanus Mwijage, (MB); Mhe. Saumu Heri
Sakala, (MB); Mhe. Salma Mohamed Mwassa, (MB); Mhe. Riziki Shahari Mngwali,
(MB); Mhe. Raisa Abdallah Mussa, (MB); Mhe. Miza Bakari Haji, (MB); Mhe. Hadija
Salum Ally Al-Qassmy, (MB); na Mhe. Halima Ali Mohamed, (MB).
Mheshimiwa Spika amejiridhisha
na maamuzi ya Mwenyekiti wa Chama hiko kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia
kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka
1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura 343 kama
ilivyojadidiwa Mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment