JESHI LA POLISI NCHINI LATOA TAHADHARI KWA WANANCHI


Jeshi la Polisi Tanzania limetoa tahadhari juu ya kundi la watu walioibuka na kufanya utapeli kwa kujifanya maafisa wa polisi kwa kigezo cha kuwapa ajira.
Imeelezwa kuwa watu hao wamesambaza taarifa kupitia mitandao ya kijamii inayosomeka vigezo sifa za kujiunga na jeshi la polisi huku ndani yake ikitaja sifa ambazo kwa mujibu wa kikundi hicho ndizo anazopaswa kuwa nazo mtu anayeomba nafasi ya kujiunga na jeshi la polisi.
Jeshi la polisi limewataka wananchi wappuuzie taarifa hizo na kwamba jeshi la Polisi lina taratibu zake na za wazi za kuajiri pale serikali inapotoa idhini ya kutangaza nafasi za ajira na kuajiri. 

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment