NEYMAR AWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI GHALI ZAIDI DUNIANI


Paris St-Germain(PSG) wamekamilisha usajili mshambuliaji wa Brazil, Neymar mwenye umri wa miaka 25, kwa ada iliyoweka rekodi mpya ya ununuzi wa mchezaji ya Euro 222m (£200m) kutoka Barcelona.
Neymar akikabidhiwa jezi namba 10 mara baada ya kutambulishwa rasmi
Rekodi hiyo imeizidi mara mbili ya rekodi iliyowekwa na mchezaji Paul Pogba ambaye alisajiliwa kwa £89m huku Neymar akiwa na dau kubwa zaidi la £200m.
Mchezaji huyo kutoka timu ya Barcelona ya Hispania ametambulishwa rasmi katika timu ya Paris St-Germain (PSG) na kukabidhiwa jezi namba kumi na Mwenyekitin waklabu hiyo, utambulisho huo umefanyika leo na umekuja mara baada ya Neymar kukubali dau nono la £200m.
Utambulisho huo umefanyika leo mara baada ya mchezaji huyo kutua nchini Ufaransa ambako ndiko makao makuu ya timu ya Paris St-Germain (PSG) akitokea nchini Hispania. Hivi karibuni imeripotiwa kwamba baadhi ya maofisa  wa ligi ya Soka ya Hispania(La Liga) kuwa wamekataa maombi ya uhamisho wa mchezaji huyo toka Barcelona kwenda Paris St-Germain (PSG).
Neymar atakuwa analipwa euro 45m (£40.7m) kwa mwaka - euro 865,000 (£782,000) kila wiki kabla ya kutozwa ushuru katika mkataba wake wa kwanza wa miaka mitano. Hiyo ni jumla ya £400m.
Rekodi ya viwango vya ada ya uhamisho tangu mwaka 1992
Neymar amesema amejiunga na mojawapo ya klabu zenye ndoto kuu zaidi Ulaya na ameahidi kufanya kila liwezekanalo kuwasaidia wachezaji wenzake.
"Ndoto kuu ya Paris St-Germain ilinivutia kujiunga na klabu hiyo, pamoja na kujitoleza kwao na nguvu zinazotokana na hili," amesema Neymar.
"Najihisi niko tayari kuanza kazi. Kuanzia leo, nitafanya kila niwezalo kuwasaidia wachezaji wenzangu wapya." Ameongeza Neymar


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment