Rais John Pombe Magufuli ameahidi
hadharani kumpatia nafasi ya juu kati ya zile atakazokuwa nazo Mkuu wa Wilaya
ya Korogwe Mhandisi Robart Gabriel kwa madai kuwa ni kiongozi anayejitoa kwa
kufanya kazi bora zinazoonekana katika
wilaya yake.
![]() |
Rais Magufuli
|
Rais ametoa ahadi hiyo leo
akiwa barabarani Hale Tanga kwenye ziara yake mkoani humo baada ya kusimama
kuzungumza na wananchi waliosimama kumpokea ndani ya mkoa huo.
Mh. Magufuli amesema kazi
anazofanya Mhandisi Gabriel ni za kuigwa kwani shughuli za maendeleo
anazozitekeleza ni kubwa kuliko hata bajeti anayopatiwa hivyo ni jambo jema kwa
kiongozi kutumia bajeti vizuri.
"Mkuu wa wilaya ya hapa
anafanya kazi sana, ni kiongozi ambaye anatekeleza miradi mingi kwa wakati na
ubora. Ameanzisha vikundi vidogo vidogo vinavyomsaidia kukamilisha miradi yake
kwa usahihi lakini pia amejenga vyumba vya madarasa vingi kuliko pesa ya
serikali iliyotolewa......Nakuahidi zile nafasi zangu za juu kama bado zipo
lazima nikupatie kwani unanifurahisha sana" alisema Rais Magufuli.
Rais ameongeza na kusema kuwa;
"Unajua watanzania
mmezoea kuwasifu watu wakishakufa, kuwa pengo lake halitazibika kumbe mnaziba
siku hiyo hiyo. Mimi namsifia kabla hajafa. nawaahidi mkuu wenu wa wilaya
nitampatia nafasi na kwa vile hata mkuu wako wa kazi amenipa ripoti nzuri
kuhusu wewe hivyo sina mashaka na wewe labda ubadilike leo baada ya
kukusifia.....Wanakorogwe sifa za kiongozi wenu ni zenu pia kwahiyo
nawapongeza." alisema Rais Magufuli
0 comments:
Post a Comment