MAREKANI NA UINGEREZA KUCHUNGUZA KIFO CHA MENEJA ICT KENYA

Marekani na Uingereza zimejitolea kusaidia uchunguzi wa mauaji ya kutatanisha ya kaimu mkurugenzi wa masuala teknolojia ya habari na mawasiliano wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC Chris Msando, kabla ya kufanyijka kwa uchaguzi mkuu.
Chris Msando
Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa balozi wa Marekani nchi Kenya Robert Godec na Balozi wa Uingereza Nic Hailey, wamelaani mauaji hayo na kuongeza kuwa wanakaribisha kujitolea kwa serikali katika kuchunguza tukio hilo.
Chris Msando alikuwa msimamizi wa mifumo ya kompiuta kwenye uchaguzi ambao utaandaliwa Jumanne, mifumo ambayo ingezuia wizi wa kura. Mwili wa Bwana Msando ulipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhia maiti jijini Nairobi siku ya Jumatatu Julai 31.
Tukio hilo limetokea ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.
Polisi wanasema kuwa mwili Msando pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo viungani mwa mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Mortuary.
Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment