SERIKALI YAMUOMBA DANGOTE KUSAIDIA KUKAMILISHA UJENZI WA KIWANDA

Tajiri wa kwanza barani Afrika Aliko Dangote, ameombwa na serikali ya Nigeria kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta kwa muda uliopangwam ambapo ujenzi umepangwa kukamilika mwaka 2019.
Aliko Dangote
Gazeti la Premium Times la nchini Nigeria lilimnukuu waziri wa mafuta Ibe Kachikwu akisema, "Rais Buhari angependa kukifungua kiwanda kikubwa kama hiki kabla ya muhula wake kukamilika"

"Ninaona tarehe ya kukamilika ujenzi wa kiwanda hiki ni Disemba mwaka 2019, lakini ninajua unaweza kuelewa kuwa ningependa mradi huu kukamilika mapema kuliko ulivyopangwa," waziri alinukuliwa akimuambia Dangote alipotembelea mradi huo mjini Lagos.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa ndicho kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta duniani kinachojengwa eneo moja na cha pili kwa kutengeneza mbolea duniani.
Licha ya kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa zaidi wa mafuta duniani, Nigeria hununua asilimia kubwa ya mafuta kutoka nje na kwa sasa inakabiliwa na uhaba mkubwa.

Wakati ujenzi wa kiwanda hicho utakamilika kitakuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kwa siku kwenda petroli, gesi ,mafuta ya taa na ya ndege.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment