Kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari,
Robert Mugabe wa Zimbabwe na marais wengine barani Africa.
![]() |
Kaguta Museven |
Bwana Buhari amekuwa akipokea
matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni
ziara ya pili anafanya kupata matibabu nchini Uingereza mwaka huu.
Lakini imekuwa tofauti kidogo kwa
rais wa miaka mingi wa Uganda Yoweri Museveni, ambaye amenukuliwa akisema kuwa
hajawai kuwa mgonjwa kwa muda wa miaka 31.
"Mshasikia kuwa Museveni ameugua
au amelazwa hospitalini kwa miaka 31 iliyipota?" aliuliza Museveni.
"Hii ni kwa sababu ninafuata
taratibu za kiafya ambazo zimenisaidia kuzuia baadhi ya magonjwa kama haya,
mengi ya magonjwa hata yanazuiwa."
Baadhi ya marais ambao pia wamesafiri
nchi za Ulaya, Asia na Marekani kupata matibabu tangu mwaka uliopita ni pamoja
na marais wa Angola, Zimbabwe, Benin na Algeria.
Rais wa Zimbabwe ambaye amekuwa madarakani
tangu mwaka 1980 amekosolewa na wapinzani kwa kuiongoza nchi "kutoka
hospitalini" baada ya kufanya ziara ya tatu nchini humo kupata matibabu
mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment