Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa,
Jeane-Pierre Lacroix, amesisitiza haja ya ushirikiano wa serikali ya Sudan
Kusini katika kuhakikisha uhasama nchini humo unafikia ukomo.
Akizungumza
na waandishi wa habari,baada ya kukutana leo hii na rais Salva Kiir katika
makao makuu ya jeshi la SPLA huko Bilpha Lacroix amesema baadhi ya mambo
waliyojadili ni kuhusu hali ya usalama akisema ameridhishwa na hatimaye
kupelekwa kwa jeshi la ulinzi wa taifa RPF, hali ya kibinadamu nchini humo,
mchango wa Uganda wa kuunganisha tena majeshi ya SPLA pamoja na umuhimu wa
kuimarisha makubaliano ya amani.
Amesema
mazungumzo na rais yamekuwa mazuri na yenye matumaini lakini kuna maeneo ambayo
bado Umoja wa Mataifa haujaridhika nayo..
“Kuhusu usalama, bila shaka, tunawasiwasi kuwa makubaliano ya
usitishaji mapigano hayatekelezwi katika maeneo yote, na rais ametueleza maoni
yake na tunatumai kuwa usalama utarejea katika maeneo yaliyoathirika, na kuhusu
hali ya kibinadamu, ni hali ambayo bado umoja wa mataifa unawasiwasi mkubwa ,
na Umoja wa Mataifa unajitahidi kutoa msaada kadri ya uwezo wake bila ya
kubagua” alisema Lacroix.
Bwana
Lacroix ameupongeza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS kwa kazi
nzuri, wadau wa masuala ya kibindamu na mashirika ya Umoja wa Mataifa na
anatarajia ushirikiano mzuri na serikali ya Sudan Kusini akisema kuwa hii ni
nchi yao na Umoja wa Mataifa upo hapo tu kuwasaidia kupata amani.
0 comments:
Post a Comment