Rais John Magufuli amesema
Tanzania imekubaliana na serikali ya Misri kuja kuanzisha kiwanda kikubwa cha
nyama ili kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili.
![]() |
Aidha, Tanzania na
Misri zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya
Kiuchumi, Elimu, Afya na Utalii.
Makubaliano
hayo ni miongoni mwa mikataba kadhaa iliyotiwa saini leo kati ya Rais Magufuli
na mgeni wake Rais Abdel Fattah – al Sisi wa Misri aliyewasili nchini leo
mchana kwa ziara ya siku mbili.
Ziara
ya Rais al – Sisi ina lengo la kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano ya
kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Misri na pia kutoa fursa
kwa viongozi hao wawili kujadili masuala mbalimbali yanaohusu nchi hizo mbili
ya kikanda na kimataifa.
Kwa
mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini, Tic, kimesajili jumla ya
miradi nane kutoka Misri kati ya mwaka 1990 hadi 2017, miradi hiyo ina jumla ya
thamani ya Dola za Kimarekani milioni 887.02 na kutoa ajira zipatazo 953,
uwekezaji huo ukiwa katika maeneo ya Kilimo, viwanda vya mbao, mbolea, madini,
na sekta ya Huduma
0 comments:
Post a Comment