Vigogo watano wa
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wanefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu leo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU wakidaiwa
kuhujumu uchumi kwa kuisababibishia serikali hasara ya takribani Milioni 275.
![]() |
Vigogo hao wa zamani
waliyofikishwa Mahakamani ni pamoja na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Tanesco, Lusekelo Kasanga, Mkurugenzi wa Fedha, Robert Shemhilu, Harun
Mattambo, Godson Makia, Ofisa Ugavi, msambazaji kutoka kampuni
ya M/S Young Dong Electronic Co. Ltd Martin Simba pamoja na Mwanasheria wao.
Hata hivyo, Wakili wa serikali Vitalis Peter
amewasomea mashtaka mawili ya uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu,Thomas Simba ambapo amedai kuwa kati ya Januari na Desemba 2011
katika Ofisi za Tanesco Ubungo, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa Shirika hilo,
walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji Martin
Simba bila ya kufanya uhakiki na kuisababishia serikali hasara ya takribani
Milioni 275.
0 comments:
Post a Comment