Siku kadhaa zimepita tangu Rais Magufuli awatake mawaziri kuwa wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka katika kazi zao, maneno hayo aliyazungumza alipokuwa ziarani kikazi jijini Tanga ambapo ilibainika kuwa mkoani humo kuna viwanda kadhaa ambavyo havifanyi kazi na kutochukuliwa hatua yoyote.
![]() |
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage |
Kufuatia hali hiyo Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, amesema serikali imeanza
utekelezaji wa awamu ya kwanza ya kutwaa viwanda walivyopewa wawekezaji na
kushindwa kuviendeleza huku viwanda vingine vikiwa chini ya uangalizi wa muda
Waziri
Mwijage amesema hayo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kumalizika kikao kilichojumuisha wawakilishi wa Wizara za Fedha,
Tamisemi na Wizara ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Watu wenye ulemavu.
Amevitaja viwanda hivyo kuwa ni
kiwanda cha korosho Lindi, Mgodi wa Pugu Kaolin, Mkata Saw Mills Ltd, Manawa
Ginnery Co Ltd, Kiwanda cha Chai Dabaga, Tembo Chipboard Ltd, Kiwanda cha Nguo
cha Kilimanjaro, Mang’ula Mechanical and Machine Tools co. Ltd na Polysacks cha
Dar es Salaam.
Aidha, Mhe. Mwijage amesema
serikali ambayo awali ilibinafsisha mashirika 341 ya umma ambayo yalijumuisha
viwanda, mashamba, makampuni ya biashara, mahoteli na makampuni ya usafirishaji
lakini kati ya hayo, viwanda vilivyobinafsishwa vilikuwa 156 huku
viwanda vinavyofanya kazi vizuri ni 62, huku viwanda vinavyosuasua vikiwa 28,
wakati viwanda visivyofanya kazi vikiwa 56 na viwanda kumi vikibinafsishwa kwa
kuuza mali moja moja.
0 comments:
Post a Comment