Mbunge wa jimbo la Chalinze,
Ridhiwani Kikwete ameahidi kuunga mkono juhudi za wafadhili na wadau wanaojitokeza kushirikiana nao kutatua changamoto mbali mbali za kimaendeleo jimboni kwake ikiwemo elimu pia amewahimiza wananchi kujenga tabia ya kujitolea katika shughuli za kimaendeleo pasipo kuachia serikali/halmashauri na wahisani pekee.
![]() |
Mbunge
wa Chalinze Mhe. Ridhiwani alitoa rai hiyo, wakati wa uzinduzi wa majengo ya
madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan Utete
iliyopo kata ya Pera, Chalinze wilayani Bagamoyo,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili
wa marafiki wa Pakistan,kwa gharama ya sh.milioni.30.
Alisema baadhi ya wafadhili
wanasaidia endapo wanaona jamii husika ikichukua juhudi na kufikia
hatua mbalimbali .
Aliwataka wananchi wa Chalinze
kushirikiana na serikali,halmashauri na wafadhili wanaojitokeza ili kukamilisha
miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao.
“Ajenda kubwa tuliyonayo ni
kuboresha na kutatua changamoto katika sekta ya elimu” alisema Ridhiwani
“Pamoja na shughuli
zinazofanywa na wahisani lakini haina budi wananchi mkajitolea katika shughuli
za maendeleo ili tukienda kuomba msaada kwa wafadhili waweze kukubali kirahisi
kwa kuona hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa“ alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alisema wakati
marafiki wa Pakistan wakiwezesha ukarabati huo,lakini halmashauri ya Chalinze
imeshatenga fedha kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo nane katika shule ya
Pakistan Utete.
Hata hivyo,mbunge huyo alieleza
kwamba,pia wanajenga matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mbala sanjali na
madarasa mawili ya shule ya msingi Makombe.
Ridhiwani alieleza,ujenzi wa
matundu ya vyoo utasaidia kuondoa kero ya uchafu wa mazingira ambapo baadhi ya
wanafunzi wamekuwa wakijisaidia ovyo maporini ,vichakani .
“Kwasasa kilichobakia ni
usimamizi katika hatua ya ujenzi unaoendelea kwenye shule hizo ”alisema
Ridhiwani.
Akizungumzia msaada walioupata
kutoka kwa marafiki wa Pakistan,Ridhiwani aliomba ushirikiano ulioonyeshwa
usiishie hapo .
Alimpongeza mwenyekiti wa
kitongoji Hussein Mramba na diwani wa kata ya Pera kwa jitihada walizozichukua
kusukuma jambo hilo.
Ridhiwani hakusita kumuomba
balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan ,kuwasaidia ujenzi wa jengo la
kulaza wagonjwa na mashine za kupima magonjwa katika kituo cha afya
Chalinze.
Akizindua majengo hayo,balozi wa Pakistan nchini Khan,alisema
amefurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania,na alishauri
kuwepo na mahusiano kati ya wabunge wa Pakistan na Tanzania.
“Nilipoambiwa kuja shuleni hapa
ni km 120 kutoka Dar es salaam nikaona nije kutembea na kuona
kilichofanyika,Nawapongeza kwa kuanzisha ujenzi huu ili watoto
wapate elimu”alisema Khan.
Alisema ili watoto hao wasome
vizuri ni vyema kukajengwa uzio katika shule hiyo ili kuweka usalama zaidi
hivyo wanatasaidia kuujenga.
Balozi huyo,aliahidi na
kukubali ombi la kusaidia mashine na vifaa vya kituo hicho cha afya lakini
kwasasa wanachotakiwa kufanya ni kuandika maombi ya msaada huo
0 comments:
Post a Comment