Bunge la Iran limepitisha muswada wa
kutenga zaidi ya dola nusu bilioni zaidi, kwa ajili ya mradi wa makombora.Iran inajibu vikwazo vya hivi karibuni vilivyowekwa na Marekani
dhidi ya nchi hiyo kufuatia vitendo vyake vya uzalishaji wa makombora ya
nyuklia.
![]() |
Vyombo
vya habari vya nchi ya Iran, vinasema kuwa fedha hizo zinakusudiwa kupambana na
vile vilivoitwa, vitendo vya kigaidi vya Marekani katika maeneo ya Mashariki ya
Kati.
|
Muswada huo utaweka vikwazo dhidi ya wanajeshi pamoja na maafisa
wa ujasusi wa Marekani.
Mpatanishi mkuu wa Iran katika mazungumzo kuhusu mradi wake wa nyuklia,
Abbas Araqchi, amesema, muswada huo mpya, umeungwa mkono na wizara ya mashauri
ya nchi za nje, na kwamba hauendi kinyume na makubaliano ya mwaka 2015,
yaliyozuia mradi wa nuklia wa Iran.
Makubaliano kuhusu mpango
wa nyuklia kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani ikiwemo China,
Urusi na Uingereza, yanaonekana kwa kiwango kikubwa kama njia mwafaka ya
kuizuia Iran kuunda zana za nyuklia.
Makubaliano hayo yalisababisha vikwazo vibaya kwa uchumi wa Iran
kuondolewa, ili nchi hiyo ipate kupunguza mipango yake ya kinyuklia.
0 comments:
Post a Comment