Maafisa nchini Somalia wanasema kuwa
mwanachama wa cheo cha juu wa kundi la al-Shabaab Moukhtar Robow amejisalimsha
kwa serikali.
![]() |
Alijisalimisha pamoja na wapiganaji wake katika mji ulio
kusini magharibu wa Hudur.
Bwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji
wake kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.
Mwezi Juni, Marekani iliondoa zawadi ya dola milioni tano
kwa bwana Robow ambaye bado anaaminiwa kuendelea na shughuli zake kama
mwanamgambo.
Al Shabab bado inathibiti maeneo makubwa ya Somalia na
kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Kenya.
0 comments:
Post a Comment