Serikali kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na Watoto imejidhatiti kujenga vyumba vya
upasuaji 170 kwa wajawazito ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto
wachanga mpaka kufikia Juni 2018.
Akizungumza hayo wakati wa
kupokea mashine ya kutoa dawa ya usingizi Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa ujenzi wa vyumba hivyo
vitasaidia kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 80 kufika 2025.
“Si tu vyumba vya upasuaji
bali tutaimarisha mahitaji muhimu ikiwemo kujenga maabara ya damu,wadi za
wazazi,tutanunua vifaa vyote vya upasuaji na kujenga nyumba moja ya watumishi
wa afya kwenye kila kituoa cha kutolea huduma ya afya” alisema Waziri Ummy.
Mbali na hayo Waziri Ummy
amesema kuwa msaada wa mashine hiyo ya kutoa dawa ya usingizi kutoka Utepe Mweupe utaisaidia kupambana kupunguza vifo vya wajawazito na watoto
wachanga kwa asilimia 40 kufikia 2020 nchini.
Aidha Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya afya kuongeza wataalamu wa kutoa dawa ya usingizi wakati Serikali ipo katika mkakati wa kuongeza vifaa na dawa kwenye vituo vinavyotolea huduma ya afya hasa uzazi.“Kama mpaka Juni mwakani tutakuwa
tumemaliza hivyo Vyumba 170 vya upasuaji
wa kutoa watoto kwa wajawazito basi Katibu Mkuu na watendaji wako mnatakiwa kuongeza wataalamu wa kutolea dawa
ya usingizi wawili kila kituo kwa hiyo jumla wawe wataalamu 340” alisisitiza
Waziri Ummy.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy
amesema kuwa Serikali imejiongeza kwa kutenga bilioni 8 kwa ajili kununua dawa
za uzazi salama ikiwemo dawa za kuzuia
kifafa cha mimba,kuzuia mama kuvuja damu na hupatikana bila ya gharama yoyote.
0 comments:
Post a Comment