Serikali
kupitia Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesaini mkataba wa ujenzi
wa awamu ya pili wa Reli ya kisasa (STANDARD GAUGE RAILWAY) kutoka Morogoro
hadi Makutupora yenye jumla ya urefu wa KM 422, ambapo ujenzi wake utagharimu
jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni 1.9 pamoja na kodi ya ongezeko la thamani
na unatarajiwa kumalizika ndani ya miezi 36.
Tukio
hilo limefanyika jana Sept 29 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere (JNICC)
jijini Dar es salaam ambapo waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa alishuhudia tukio hilo la utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa reli hiyo, ambapo Mkurugenzi wa Shirika la Reli na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za
Reli Ndg. Masanja Kadogosa na Mkurugenzi wa Kampuni ya YAPI iliyoshinda kandarasi
hiyo kutoka Uturuki waliweka saini makubaliano hayo.
Lakini
pia mradi huu utahusisha ujenzi wa wigo wa wa njia ya reli kutoka Morogoro hadi
Makutupora, ujenzi wa vivuko vya watembea kwa miguu, magari pamoja na sehemu
maalum za kuvushia mifugo. Aidha reli hii itakuwa na uwezo wa kuhimili hadi
tani 35 kwa ekseli, na kupitisha treni zenye uwezo wa kwenda mwendokasi wa
Kilometa 160 kwa saa.
0 comments:
Post a Comment