Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole ametoa
ufafanuzi kuhusu sababu zilizomfanya katibu mkuu wa chama hiko Mhe. Abdulrahman
Kinana kutohudhuria kikao cha kamati kuu ya Chama hiko kilichofunguliwa na
Mwenyekiti wake Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Katibu wa itikadi na
uenezi wa CCM Humphrey Polepole
|
Polepole ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi ndogo za chama cha Mapinduzi, Lumumba jijini Dar es salaam
na kusema kwamba katibu mkuu wa chama hiko Abdulrahman Kinana ameshindwa
kuhudhuria kikao hiko kutokana na kuuguliwa na mwanafamilia wa karibu lakini
alikuwepo wakati wa maandalizi ya mkutano huo.
"Katibu Mkuu Kinana
anauguza mwanafamilia, ni mambo ya kifamilia lakini alikuwapo wakati wa maandalizi
ya mkutano hadi mwisho," alisema Polepole
Aidha Polepole
amekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya watu kuhusu Kinana, ya kwamba
ameandika barua ya kujiuzulu, Polepole amesisitiza taarifa hizo kuwa ni za
uzushi.
0 comments:
Post a Comment