Ndege ya kijeshi imeanguka nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na kuwaua abiria wote waliokuwamo kwenye ndege hiyo
asubuhi ya leo.
Maafisa wa maswala ya anga wamesema kuwa ndege hiyo ilishindwa kupaa
vizuri kutoka uwanja wa ndege wa N'djili katika mji mkuu wa Kinshasa na
kuanguka katika makaazi ya Nsele.
Taarifa za awali kutoka mamlaka ya anga na maofisa wa jeshi wa DRC
zimesema kuwa watu 12 wamefariki baada ya ndege hiyo ya mizigo ya Jeshi
kuanguka muda mfupi baada ya kuruka
Taarifa PIA zimeeleza kwamba ndege hiyo ilikuwa imebeba magari mawili,
silaha, raia kadhaa kutoka Urusi pamoja na maofisa wa kijeshi wa Congo
Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kinshasa George Tabora
amesema kuwa ndege hiyo ilikuwa iimebeba mizigo na kwamba haikuwa na
abiria wowote, "ndege
hiyo haikuwa ikisafirisha abiria na hakuna aliyenusurika kwenye ajali hiyo" alisema Tabora
0 comments:
Post a Comment