Mkutano mkuu wa CCM taifa (NEC)
umefuta uchaguzi wa wenyeviti katika wilaya nne baada ya kubaini wagombea waliojitokeza
hawakuwa na sifa.
Akitangaza uamuzi huo leo
katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole amezitaja wilaya hizo kuwa
ni Moshi Mjini, Siha, Hai pamoja na Makete, "Nafasi za uenyekiti Wilaya za
Hai, Siha, Makete na Moshi Mjini zitatangazwa tena wagombea wana kasoro
kimaadili" amesema Polepole
Amesema sababu ya kufuta
matokeo hayo ni kubainika kwamba wagombea waliojitokeza hwakuwa na sifa, pamoja
na kubainika kuwepo kwa viashiria hatarishi kwa chama.
Aidha Polepole ameeleza hali
ya uchaguzi wa chama hiko nchi nzima na kusema kuwa uchaguzi kwa ngazi ya
mashina na matawi na kata umefanikiwa kwa asilimia 97, "Kwa nchi nzima CCM ina mashina zaidi ya laki 2 na 22
elfu na matawi zaidi ya 23 elfu Chaguzi zimekamilika zaidi ya 97%" amesema
Polepole
0 comments:
Post a Comment