SPIKA NDUGAI AKANUSHA KAULI YA MBOWE KWA WAANDISHI WA HABARI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amjibu Freeman Mbowe, asema pesa za wabunge zilizochangishwa kwa ajili kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu tayari zimetumwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikolazwa Tundu Lissu kwa matibabu.

Taarifa hiyo imefuatia mara baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe kusema kwamba pesa zilizochangishwa na wabunge kwa kutoa nusu ya posho yao ya siku bado haijawasilishwa, Mbowe aliyazungumza hayo alipokuwa katika mkutano wake na waandishi wa habari leo kuzungumzia hali na muenendo ya matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana wiki kadhaa zilizopita jijini Dodoma.

Taarifa hiyo ya Bunge imeeleza kuwa jumla ya Tsh. Milioni 43 zilichangishwa bungeni na wabunge kwa kutoa nusu ya posho zao za siku moja, zilitumwa siku ya tarehe 20 Septemba 2017 kupitia benki ya Barclays tawi la Hurlringam kwenye akaunti Namba. 045 1155318

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment