Mgomo mkubwa umeitishwa na vyama vya wafanyakazi
huko Catalonia baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi ya ukiukwaji
mkubwa wa haki za binadamu ulioshuhudiwa wakati wa kura ya maoni ya siku ya
Jumapili, mgomo huo unatishia kukwamisha shughuli sehemu kubwa za Catalonia
kufuatia kura ya maoni yenye utata nchini Uhispania.
Mamlaka nchini Uhispania zimeitaja kura hiyo ya
maoni kuwa iko kinyume na sheria. Hata hivyo zaidi ya watu milioni 2.2 walipiga
kura huku zaidi ya asilimia 90 ya waliopiga kura hiyo walitaka uhuru wa eneo hilo upatikane
ili waweze kujitenga na nchi ya Uhispania.
Aidha mamia ya watu wameripotiwa kujeruhiwa wakati
polisi wa Uhispania walipokuwa wakijaribu kuzuia zoezi hilo kuendelea, ambapo
ilielezwa kuwa askari walitanda kila kukabiliana na watu waliofanya zoezi hilo siku ya Jumapili.
Baadhi
ya maafisa walioamrishwa kuwazuia watu wasipige kura walionekana wakifyatua
risasi za mipira, wakivamia vituo vya kupigia kura, kuwapiga watu kwa virungu na kuwavuta wanawake kwa
nywele zao.
Polisi watatu walijeruhiwa siku ya Jumapili, kwa mujibu wa maafisa wa afya huko Catalonia.
Mgomo huo wa leo Jumanne utavuruga shushuli za usafiri wa umma, shule na
zahahati huko Catalonia.
Klabu
maarufu ya soka ya Barcelona pia inatarajiwa kugoma, licha ya kuwa
hawachezi mechi huku vyuo vya umma na makavazi nayo yakitarajiwa kugoma.
Wachezaji wa timu hiyo walionekana siku ya Jumapili wamevalia mavazi ya
kuashiria kutaka uhuru wa eneo hilo la Catalona.
Ramani ikionesha mipaka na eneo la Catalona. |
0 comments:
Post a Comment