Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua makumbusho ya Olduvai Gorge, ambako
ni chimbuko la historia ya binadamu. Samia
amesema kuwa makumbusho hayo ni kielelezo cha maisha na ustaarabu wa binadamu
ambao unaelezea maisha ya vizazi vilivyopita, na kusaidia kujua hasa historia
ya binadamu. Pia ameongeza kuwa ujenzi wa makumbusho hayo utasaidia kuvutia watalii
na wanasayansi wa masuala ya mambo kale duniani.
“Makumbusho
haya pia yatasaidia kujua sisi ni nani na tumetoka wapi,” amesema Makamu wa
Rais.
Samia
amesema eneo la Ngorongoro lina historia kubwa ya maisha ya zamadamu ikibainika
miaka 3 milioni iliyopita walikuwepo walioishi kwa kutembelea miguu miwili na
kuahidi kuwa serikali itaendelea kulihifadhi na kulilinda eneo hilo.
“Hapa ni chimbuko la historia ya zamadamu,
Serikali itaendelea kulihifadhi na kulitunza eneo hili,” amesema.
Makamu
wa Rais ameishukuru Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa fedha kugharimia ujenzi wa
makumbusho hayo na miundombinu yake.
Makamu
wa Rais ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro kuwa na mkakati wa kutangaza makumbusho hayo ndani na nje ya nchi
ili kuvutia zaidi watalii.
Pia,
amewaomba wananchi wa Ngorongoro kuendelea kuhifadhi eneo hilo ikiwemo
kutopeleka mifugo eneo la Creta. Amesema Serikali inajitahidi kuwaondolea kero
zao likiwemo tatizo la maji.
0 comments:
Post a Comment