Askofu wa Kanisa la Ufufuo
na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema kuwa Jumatano hii atatembelea Clouds
Media Group kwajili ya kuwapa pole kwa yaliyotokea hivi karibuni.
Ijumaa
iliyopita kituo hicho kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
akiwa na askari wenye mitutu kitendo kilichopingwa na wadau mbalimbali wa
habari.
“Kesho
Tarehe 22/03/2017 saa nne kamili asubuhi, nitatembelea Ofisi za Clouds Media
ili kuwapa pole kwa yaliyotokea.” aliandika mchungaji huyo kupitia ukurasa wake
wa Instagram.
0 comments:
Post a Comment